Karibu mtu wa MUNGU, utafakari ujumbe huu mfupi.
Ujumbe wa leo unasema AHADI HII SIYO YA KUKOSA.
Kuna ahadi nyingi sana hapa duniani tunaahidiwa, nyingine huwa zinatimia na nyingine huwa hazitimii.
Ni kawaida ya mwanadamu kutoa ahadi lakini ni mara chache sana kutimiza alichoahidi.
Lakini katika zote ipo ahadi moja nzuri sana ambayo ipo hapa duniani tumeahidiwa watu wote na lazima itimiye. Nasema ni lazima maana aliyeahidi ni YESU.
Ahadi hii ni ya uhakika maana Biblia inasema katika HESABU 23:19
"Mungu si mtu, aseme uongo; Wala si mwanadamu, ajute; Iwapo amesema, hatalitenda? Iwapo amenena, hatalifikiliza?
Unaweza kuwa unajiuliza ni ahadi gani hiyo.
Ahadi yenyewe hii hapa.



Yohana 14
1 Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. 2 Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia;
6 Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
Oh! Haleluya!!! Yesu anasema ameenda kutuandalia makao, atakuja tena atukaribishe kwake ili tukae pamoja naye.
Kumbuka ahadi hii ni kwa wanadamu wote. YESU alikuja hapa duniani kuwaokoa wote ili kila amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele. Tunaoma katika YOHANA 3:16
"Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele."
Lakini ili na wewe itimie kwako ni lazima uijue njia.
Ukisoma mstari wa sita unasema YESU ndiye njia, kweli na uzima. Kwa hiyo kama hujamwamini YESU basi utakua unachengana na hii ahadi.
YESU yupo karibu kurudi, Je? Atakukuta kwenye njia? Yaani umemwamini.?
Je? Atakukuta na utakatifu? Maana wasio watakatifu hawatamuona MUNGU. (EBR 12:14) Inasema
"Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao"
Wala vinyonge havitaingia mbinguni. (UFUNUO 21:27) Inasema
"Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo."


UBARIKIWE.
Ni mimi ndugu yako Faraja Euphrase
© farajaefraz@gma
No comments:
Post a Comment