No copying

Saturday, 13 May 2017

MANENO YANAUMBA


Karibu tujifunze neon la MUNGU.

Naomba tujifunze kwa habari ya maneno tunayotamka kila siku. Katika kinywa cha mtu asipokuwa makini, atakuwa anajibariki mwenyewe au atakuwa anajirahani mwenyewe.

Uwe makini sana kwa yale unayotamka, kwa maana maneno huumba. Tumeumbwa kwa mfano wa Mungu kiroho, Mungu aliumba kwa neno.


1 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.
2 Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.
3 Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.
YOHANA 1:1'

Kwa hiyo hata wewe kwa jinsi unavyotamka unaumba. Kama maneno yako ni ya baraka utaanza kuona Baraka kama ni ya laana utaanza kuona mikosi na balaa.
Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yakeMITHALI 18:21).

Unajua wako malaika ambao wametuzunguka ambao kazi yao ni kuchukua kila maneno tunayotamka yawe ni mabaya (ya laana) au mazuri (ya baraka)
Usikiache kinywa chako kuukosesha mwili wako; wala usiseme mbele ya huyo malaika ya kwamba umepitiliwa; kwani Mungu akukasirikie sauti yako, na kuiharibu kazi ya mikono yako? MHUBIRI 5:6) 
Mfano ukisoma injili ya Luka, utaona pia YESU alikuwa anategwa kwa kuulizwa jambo ili waone atajibuje waweze kumshtaki. Mfano pia katika YOHANA 8:6 Inasema hivi " Nao wakasema neno hilo wakimjaribu, ili wapate sababu ya kumshitaki. Lakini Yesu akainama, akaandika kwa kidole chake katika nchi."
Unafikiri kwa nini YESU aliandika chini badala ya kuwambia kwa maneno.
Neno la Mungu pia linasema " Basi, nawaambia, Kila neno lisilo maana, watakalolinena wanadamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu. Kwa kuwa kwa maneno yako utahesabiwa haki, na kwa maneno yako utahukumiwa." (MATAYO 12:36-37)


Neno lipo wazi hapo juu, ndiyo maana nasema uwe makini sana katika kutamka maneno yako, kwako wewe mwenyewe, au kwa wengine.
Usipende kutamka kushindwa bali tamka maneno ya ushindi muda mwingine mtu anaweza kukumtamkia maneno yw kushindwa, kataa hapo hapo baada ya kutamka.

Mfano mtu anakuja anakwambia "hii biashara uliyoianzisha huiwezi ndugu yangu" Mwambie hivi "nayaweza yote katika yeye anitiaye nguvu"
Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu. WAFILIPI 4:13


 
 

Kuwa makini mpendwa usije ukakamatwa kwa maneno yako.
Basi umetegwa kwa maneno ya kinywa chako, Umekamatwa kwa maneno ya kinywa chakoMITHALI 6:2

Ni mimi ndugu yako katika Kristo farajaefraz@gmail.com
0757628749

No comments:

 

Top

Back To Top
 
Blogger Templates