UAMINIFU ni kitu cha msingi sana katika maisha ya MWAMINI.
Iwe ni katika matakatifu ya MUNGU au katika mambo mengine tu ya kawaida.
UAMINIFU huvuta BARAKA zako mahali zilipo.
*MATENDO 5*
Lakini mtu mmoja jina lake Anania, pamoja na Safira mkewe, aliuza mali,
akazuia kwa siri sehemu ya thamani yake, mkewe naye akijua haya, akaleta fungu moja akaliweka miguuni pa mitume.
Lakini mtu mmoja jina lake Anania, pamoja na Safira mkewe, aliuza mali,
akazuia kwa siri sehemu ya thamani yake, mkewe naye akijua haya, akaleta fungu moja akaliweka miguuni pa mitume.
Petro akasema, Anania, kwa nini Shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho Mtakatifu, na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya kiwanja?
Kilipokuwa kwako, hakikuwa mali yako? Na kilipokuwa kimekwisha kuuzwa, thamani yake haikuwa katika uwezo wako? Ilikuwaje hata ukaweka neno hili moyoni mwako? Hukumwambia uongo mwanadamu, bali Mungu.
Anania aliposikia maneno haya akaanguka, akafa. Hofu nyingi ikawapata watu wote walioyasikia haya.
*ANGALIA WAAMINI WALIVYO.*

Nimetoa huo mfano mmoja tu lakini ipo mingi sana ya namna hiyo.
Mpendwa usitumie kitu ambacho hujaambiwa utumie hata kama ni kidogo rudisha mahali husika, kama wao watakwambia chukua itakuwa ni vizuri kuliko kujichukulia maamuzi yako tu.
ANANIA alikufa. Inawezekana unajiona hujafa lakini maana ya kufa inaweza kwenda hadi katika kufa kwa Baraka zako au maisha yako yote yakawa siyo ya maendeleo maana tayari kuna kifo.
By Faraja Euphrase
No comments:
Post a Comment