Karibu tujifunze neon la MUNGU.
Kuna siku asubuhi nilikutana na mama mmoja jirani yangu. Kama kawaida huwezi kumpita mtu bila kumsalimia. Yafuatayo ndiyo tuliyoongea huku tumesimama kwa heshima:-
MIMI: Shikamoo Mama...
MAMA: Marahabaa!!!!! Hujambo.
MIMI: Sijambo! Kumekucha.
MAMA: Ndiyo; na makucha yake.
MIMI: Hapana Mama kumekucha na Baraka zake.
MAMA: Te te te te ……(Akacheka)
MIMI: Usicheke.
MAMA: Kwa hiyo nimekosea kusema "Makucha"?
MIMI: Ndiyo! Maana makucha ni ya shetani..lakini
MAMA: Hivooo!! (akaitikia kipwani pwani)
Basi nikaendelea kumuelezea pale kwa jinsi anavotamka hayo maneno ni nini huwa anachojitabilia
Nilishawahi kupost kitu kama hiki kwamba angalia sana unatamka nini, na unakili nini.
Maneno huumba, na ulimi ni kiungo kidogo lakini matatizo yake ni makubwa.
Ngoja tuangalia haya maandiko yanavyozungumza kwa habari ya ulimi:-
Zaburi 39:1 Nalisema, Nitazitunza njia zangu Nisije nikakosa kwa ulimi wangu; Nitajitia lijamu kinywani, Maadamu mtu mbaya yupo mbele yangu.
Zaburi 52:2 Ulimi wako watunga madhara, Kama wembe mkali, Ewe mwenye hila
Mithali 6:17 Macho ya kiburi, ulimi wa uongo, Na mikono imwagayo damu isiyo na hatia;
Mithali 10:20 Ulimi wa mwenye haki ni kama fedha teule; Moyo wa mtu mbaya haufai kitu.
Mithali 10:31 Kinywa cha mwenye haki hutoa hekima; Bali ulimi wa ukaidi utakatiliwa mbali
Mithali 12:18 Kuna anenaye bila kufikiri, kama kuchoma kwa upanga; Bali ulimi wa mwenye haki ni afya.
Mithali 12:19 Mdomo wa kweli utathibitishwa milele; Bali ulimi wa uongo ni wa kitambo tu.
Mithali 15:2 Ulimi wa mwenye hekima hutamka maarifa vizuri; Bali vinywa vya wapumbavu humwaga upumbavu.
Mithali 15:4 Ulimi safi ni mti wa uzima; Bali ukorofi wa ulimi huvunja moyo.
Mithali 17:20 Mtu mwenye moyo wa ukaidi hatapata mema; Na mwenye ulimi wa upotofu huanguka katika misiba.
Mithali 8:21 Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake.
Mithali 21:6 Kupata akiba ya mali kwa ulimi wa uongo Ni moshi upeperushwao; ni kutafuta mauti.
Mithali 21:23 Mtu azuiaye kinywa chake na ulimi wake, Atajilinda nafsi yake na taabu.
Mithali 26:28 Ulimi unenao uongo huwachukia wale uliowajeruhi; Na kinywa cha kujipendekeza hutenda uharibifu.
Jeremia 9:8 Ulimi wao ni mshale ufishao; husema maneno ya hadaa; mtu mmoja husema maneno ya amani na mwenzake kwa kinywa chake, lakini moyoni mwake humwotea.
Yakobo 3:5 Vivyo hivyo ulimi nao ni kiungo kidogo, nao hujivuna majivuno makuu. Angalieni jinsi moto mdogo uwashavyo msitu mkubwa sana.
Yakobo 3:6 Nao ulimi ni moto; ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi, umewekwa katika viungo vyetu, nao ndio uutiao mwili wote unajisi, huuwasha moto mfulizo wa maumbile, nao huwashwa moto na jehanum.
Yakobo 3:8 Bali ulimi hakuna awezaye kuufuga; ni uovu usiotulia, umejaa sumu iletayo mauti.
1Petro 3:10 Kwa maana, Atakaye kupenda maisha, Na kuona siku njema, Auzuie ulimi wake usinene mabaya, Na midomo yake isiseme hila
Ni mimi ndugu yako Faraja Euphrase
0757628749 ULIMI UNATAWALA MWELEKEO WA MAISHA YAKO.
No comments:
Post a Comment