![]() |
YESU ndiyo MUNGU aliye hai. |
Karibu mtu wa MUNGU tujifunze neon la MUNGU.
Biblia takatifu inasema MUNGU anawapenda wale wampendao tu; kama humpendi MUNGU ina maana hawezi kukupenda pia.
- Nawapenda wale wanipendao, Na wale wanitafutao kwa bidii wataniona. -MITHALI 8:17
- Mkinipenda, mtazishika amri zangu.- YOHANA 14:15
- Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito. -1YOHANA 5:3
- Awapokeaye ninyi, anipokea mimi; naye anipokeaye mimi, ampokea yeye aliyenituma (MUNGU).---MATHAYO 10:40
- Awasikilizaye ninyi (watumishi wa Mungu) anisikiliza mimi, naye awakataaye ninyi anikataa mimi; naye anikataaye mimi amkataa yeye aliyenituma.---LUKA 10:16
>>Huwezi kuseme unampenda MUNGU wakati unamchukia YESU.
- Yeye anichukiaye mimi humchukia na Baba yangu.--YOHANA 15:23
- Ili watu wote wamheshimu Mwana kama vile wanavyomheshimu Baba. Asiyemheshimu Mwana hamheshimu Baba aliyempeleka.--YOHANA 5:23
Lakini nina neno moja kwako wewe ambaye hujaokoka au hujamwamini YESU.
Amua kumfuata na kumuamini ili upate uzima.
Ni mimi ndugu yako Faraja Euphrase
0757628749
farajaefraz@gmail.com
No comments:
Post a Comment