No copying

Saturday, 13 May 2017

IWENI WEPESI WA KUSAMEHE




Karibu mtu wa MUNGU tujifunze neon la MUNGU.
Biblia inasema
" Patana na mshitaki wako upesi, wakati uwapo pamoja naye njiani; yule mshitaki asije akakupeleka kwa kadhi, na kadhi akakupeleka kwa askari, ukatupwa gerezani. ~ Matayo 5:25.





Lengo la kuomba msamaha ni kurejesha amani na furaha. Siyo juu ya nani kakosea na nani yuko sahihi. Ikitokea umemuudhi au umemuumiza mtu yeyote (labda mkeo) juu ya jambo flani; hakikisha unafanya njia yoyote kwa haraka sana ili umfanye ajisikie vizuri na kurudi katika hali yake ya kawaida.
Kumbuka kusamehe ni gharama lakini ni faida kwako, na ukisamehe usahau. Haiwezekani umwambie mtu "nimekusamehe ila sitasau" yani hapo ni kama hujasamehe.

 Neno la Mungu linasema hivi; " Msihukumu, nanyi hamtahukumiwa; msilaumu, nanyi hamtalaumiwa; achilieni, nanyi mtaachiliwa."~LUKA 6:37) Hayo ni maneno ya YESU mwenyewe, usipende kumbeba mtu moyoni mwako bali hakikisha unaachili. Dalili ya kumbeba mtu ni pale unapomuona alafu unakumbuka jinsi alivyokukosea/ulivyomkosea.

Kusamehe hakuna mipaka hata kama mtu anakukosea kila siku, neno la Mungu linasema; " 21 Kisha Petro akamwendea akamwambia, Bwana, ndugu yangu anikose mara ngapi nami nimsamehe? Hata mara saba?
22 Yesu akamwambia, Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini."
~MATAYO 18:21~22


 Ili ibada yako iwe safi mbele za Mungu na yenye kibali lazima uhakikishe umesamehe yeyote aliyekukosea.
Leo hii kuna watu wanaenda kanisani lakini yeye na jirani yake hawapatani, mke na mme wamegombana lakini wanaenda kanisani na wakiwa kanisani unasema hii ndoa ina amani lakini kimsingi wakifika nyumbani ni ugomvi tupu.
Neno la Mungu linasema;
"Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu.
Lakini kama ninyi hamsamehe, wala Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu."
~MARKO 11:25~26



 Kusamehe ni lazima ili usamehewe kama tuliona huo mstari wa juu. Ili Mungu ajibu maombi yako lazima usamehe wengine. Neno la MUNGU linasema
1 Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia;

2 lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.

3 Kwa maana mikono yenu imetiwa unajisi kwa damu, na vidole vyenu vimetiwa unajisi kwa uovu; midomo yenu imenena uongo, ndimi zenu zimenong'ona ubaya.---ISAYA 59:1-3

Ubarikiwe kwa kusoma ujumbe huu.
Ni mimi ndugu yako Faraja Euphrase
0757628749

No comments:

 

Top

Back To Top
 
Blogger Templates