No copying

Saturday, 3 June 2017

UMFANYIALO; LITAKUPATA

UMFANYIALO; LITAKUPATA.

Karibu mtu wa MUNGU tjifunze neno la MUNGU japo kwa ufupi.

Neno la MUNGU linasema katika ISAYA πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡




 Isaya 33
1  Ole wako uharibuye ila hukuharibiwa, utendaye hila wala hukutendwa hila! Utakapokwisha kuharibu, utaharibiwa wewe; na utakapokwisha kutenda kwa hila, wao watakutenda hila wewe.

Duu! Biblia ukiifatilia lazima ikufungue tu ufahamu wako.

Kuna watu bana kazi yao ni kuwaonea wengine, kuwatenda wenzake vibaya, lakini wao hawakutendewa vibaya,  laiti kama wangejua neno hili.
Neno likufungue mfahamu wako na ujue hivyo kwamba kumbe ukimtenda mwenzio nawe ipo aiku utatendwa.

Kumbe basi yawezekana kuna mambo mengine mabaya humapata mtu ni kwa sababu labda aliwahi na yeye kuwatendea wenzake ila amesahau ndo maana analalamika kwa nini nimefanyiwa hivi?
Kuna msemo mmoja unasema malipo ni hapa hapa duniani. Ule msemo nahisi ulitokana na hili neno.

πŸ‘‰ Ukichukua mme wa mtu na wako atachukuliwa.
πŸ‘‰ Kama unatabia ya kuwaonea na kuwatendea vibaya watoto wa jirani zako; na wako watatendewa vivyo hivyo.
πŸ‘‰ Unachukua wake za watu; na wako jamaaa watachukua.

Yani hiyo ndiyo  formula.


Tuangalie tena UFUNUO 13:10 πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

 10  Mtu akichukua mateka, atachukuliwa mateka. Mtu akiua kwa upanga, atauawa kwa upanga. Hapa ndipo penye subira na imani ya watakatifu.

 Sitaki kuongezea maelezo mengi sana.
Ila naupenda huo mstari wa 10c. Yani kwa watakatifu, hapo ndipo ilipo subira. Ndiyo maana hawanaga visasi, yani ukimdhurumu hakudai, ukimpiga hakurudishii maana anajua tu kama umepiga wakatu yeye hajakupiga, basi utapigwa na wewe.
Na anajua kisasi ni cha MUNGU mwenyewe. πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

 Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana. RUM 12:19
Tuangalie ZABURI 109:17πŸ‘‡πŸ‘‡
 17  Naye alipenda kulaani, nako kukampata. Hakupendezwa na kubariki, kukawa mbali naye,


Iyo Zaburi kama inatoa taarifa ya mtu flani kwamba alilaaniwa kwa sababu alipenda kulaani.
Napenda sana unielewe nini namaanisha najua unanielewa.

Yani kwenye maisha usifanye kitu eti umkomoe mwenzako, utakuwa unajikomoa mwenyewe.

Unakumbuka pia YESU alisemaje pale mwanafunzi wake alipomkata mtu sikio walipotaka kumkamata. πŸ‘‡πŸ‘‡

 52  Ndipo Yesu akamwambia, Rudisha upanga wako mahali pake, maana wote waushikao upanga, wataangamia kwa upanga. MATHAYI 26:52

Naishia hapo kwa leo mbarikiwe na BWANA, mwenye masikio na asikie.
Tchao…πŸ™‹πŸ»‍♂

No comments:

 

Top

Back To Top
 
Blogger Templates