No copying

Tuesday, 24 October 2017

SHETANI HAJAFA.

Hapo mwanzo shetani alikuwa na nafasi nzuri sana mbele za MUNGU kabla hajamuasi MUNGU. Lakini baada ya kuasi kwa kiburi alichofanya mbele za MUNGU akatupwa chini (duniani).




Baada ya kutupwa alipata hasira sana na akasema atahakikisha anamsumbua mwanadamu aliyeko duniani kwa kuvuruga mambo yake na maisha yake kwa ujumla.

Ndiyo maana baada ya kuona Adam anapata raha pale bustanini akaamua aende kuharibu kile ambacho MUNGU alikuwa amewapa Adam na Hawa.

Ndivyo ilivyo hata leo, kuna mtu atakuja kwako kwa kukuletea habari za uongo juu ya mtu flani ambaye anaona kupitia yeye wewe unabarikiwa au utabalikiwa. Atakuja kwako kama alivyoenda kwa Hawa na kuanza kumdanganya lengo hasa likiwa ni kwamba akifanikisha mpango wake basi yale ambayo unapata au ungepata kwa mtu flani huyapati tena.

Kama MUNGU anamtumia shetani kufikisha ujumbe wake kwa wanadamu, ndivyo ilivyo hata kwa shetani; naye humtumia mtu kufanya uharibifu wake kwako.

Kuna mtu atakuja kwako kuleta habari za uongo akisema "unajua flani yuko hivi na hivi kwa hiyo usiwe karibu naye wala usifanye naye kabisa yale ambayo ulikuwa ufanye naye( yaweza kuwa ni biashara au mambo mengine ya msingi kabisa.) Pale utakapoamua kumsikiliza tena hata bila kuwa na uhakika na hicho unachoambiwa, ndipon hapo shetani anakuwa amefanikiwa kusudi lake.

Kuna watu watakuja kwako unawaona kama watu lakini kimsingi ni shetani, maana kile anachokitoa ndani yake kimetoka kwa shetani.

YOHANA 10:10 Inasema kazi ya shetani ni kuua nakuharibu tu.

Unapoambiwa jambo hakikisha unachunguza kupata uhalisia wake, wakati mwingine muulize MUNGU, maana yawezekana limetoka kwa MUNGU au kwa shetani (baba wa oungo).

No comments:

 

Top

Back To Top
 
Blogger Templates