No copying

Sunday, 16 July 2017

ANZA KWANZA KUUTAWALA ULIMWENGU WA ROHO



Karibu mwana wa MUNGU tujifunze. Leo tunaangalia somo linasema KUUTAWALA KWANZA ULIMWENGU WA ROHO.
Nini maana ya ulimwengu wa roho?
Ulimwengu wa roho ni ulimwengu usioonekana kwa macho ya damu na nyama. Ulimwengu wa roho ni ulimwengu halisi kama ilivyo hii dunia. Mapepo, majini yanaishi katika huo ulimwengu ndiyo maana huwa hatuyaoni. Wachawi na waganga hufanikisha mambo yao kwa namna ya rohoni yaani katika ulimwengu wa roho.


Mungu huongea na watu wanaoona,ndiyo sababu Mungu kwenye biblia alikua anakawaida ya kuwauliza watu unaona nini. Kutawala kunaanzia kwenye ulimwenguu wa roho na kushindwa pia kunaanzia  katika ulimwengu roho. Hapa namaanisha kila kitu huanzia katika ulimwengu wa roho kabla hakijadhihirika katika ulimwengu wa damu na nyama.

Waebrania 11:3

"Kwa Imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu hata vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri"

Kila vinavyoonekana vimetokana na vile visivyoonekana,mafanikio ya mwilini yanatokana na mafanikio yaliyoanzia kwenye ulimwengu usioonekana yaani ulimwengu wa roho.Ndiyo sababu vile visivyooonekana ni vya kudumu milele na vinavyoonekana ni vya muda tu.

2 Wakorintho 4:16-18 “…tusiviangalie vinavyoonekana,bali visivyoonekana.kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu,bali visivyoonekana ni vya milele"
Tuangalia sasa katika Uumbaji wa Mungu, Je? Adamu alianzia wapi?
Mwanzo 1 : 26 - Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
Mwanzo 1 : 27 - Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.

Mwanzo 2 : 7 - Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.
Tumeona mara ya kwanza MUNGU aliwaumba me na ke. (Mwanzo 1:26~27). Alafu katika andiko la pili ndipo tunaona sasa MUNGU anamfanya mtu kwa mavumbi (udongo). Hapa sasa ndipo tunaona mtu anakuwa katika mwili. (MWANZO 2:7).
Kumbuka uyo mtu MUNGU alimuita Adamu.
MWA 1:27, tumeona MUNGU aliumba me na ke. Je? Adamu alikuwa na jinsia gani?
Kwa maadiko yale mawili, inadhihirisha kuwa kuwa Adam wakati amekuwa katika mwili alikuwa na jinsia mbili
Namaanisha hivi ke ilikuwa ndani ya me lakini katika ulimwengu wa roho
Ndiyo maana sasa baadae tunaona baada ya MUNGU kuona Adam hana msaidizi alitwaa ubavu mmoja kwa Adamu akamfanya mwanamke, ambaye ni Hawa.
Hadi hapo sasa tumeona hata mwanadamu alianzia katika ulimwengu usioonekana.
Kwa kifupi naweza kusema kuwa, mwanadamu halisi ni roho (maana ndiyo iliyoanza kuumbwa MWA 1:27). Huu mwili ulionao umeibeba tu ile roho.
Angalia andiko hili.
 Na kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu. Na hii ndiyo roho ya mpinga Kristo ambayo mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani.
1YOH 4:3
Point yangu ipo hapo kwenye "kila roho isiyomkiri YESU haitokani na MUNGU".
Ndiyo maana nasema mwanadamu halisi ni yule wa ndani asiyeonekana, maana mtu anaweza kwa nje akakwambia nampenda YESU, lakini kumbe rohoni mwake hana YESU.
Kwa hiyo kama mwanadamu ni roho, na kila kitu kinaanzia rohoni, basi hata baraka zako zinaanzia rohoni, mafanikio yako yananzia rohoni, uzima wako pia ni katika roho nk.
Kama ndivo ilivyo, ni lazima tuhakikishe tunautawala ulimwengu wa roho.```
Waefeso 1 : 3 - Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo;
3 Yohana 1:2
  Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo.
Ukiviangalia vile visivyoonekana tunapata ufumbuzi wa milele na tunapoviangalia vile vinavyoonekana tunapata ufumbuzi wa muda tu.Vitu vinavyoonekana vinakua na ufumbuzi wa muda tu lakini vitu vile visivyoonekana vinakawaida ya kutokua na mipaka. 

1Wakorintho 2:9
"lakini kama ilivyoandikwa,mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia (wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu). Mambo hayo Mungu aliwaandalia wampendao."

Mambo ambayo hata hujawahi kuyawaza wala jicho halijawahi kuyaona, mambo hayo Bwana amewaandalia wampendao, Kama vitu vinaanzia kwenye kutokuonekana tunatakiwa kung’ang’ania kwenye vile visivyoonekana ili kupokea majibu yetu yenye kuonekana.

Yeremia 1:11
Tena neno la Bwana likanijia kusema, Yeremia, waona nini?. Nikasema ninaona ufito wa mlozi, ndipo Bwana akaniambia umeona vema, kwa maana ninaliangalia neno langu ili nilitimize. 
Bwana anaongea na wale wanaoona vitu,ukiona ushindi,ushindi unatokea kwako,ukiona ufumbuzi ufumbuzi unatokea kwako,ukiona taabu, taabu inatokea kwako.

Hata  vita tunayopigana ni katika ulimwengu usioonekana, mambo yasiyoonekana yanasababisha mambo yanayoonekana.
Waefeso 6:12
“kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama….katika ulimwengu waroho”
Unaposhinda rohoni ushindi unaonekana mwilini na unapopigwa rohoni na mwilini unashindwa, kwa sababu majeshi tunayopambana nayo yako katika ulimwengu wa roho.

NAFASI YAKO ROHONI.
Kila mtu aliyeokoka anayo nafasi yake katika ulimwengu wa roho,
Waefeso 1:3
  “…aliyetubariki kwa Baraka zote za rohoni katika ulimwengu waroho katika Kristo Yesu.
Hatuhitaji kumwambia Mungu atubariki kwasababu Mungu ameshatubariki kwa baraka zote katika ulimwengu wa roho, biblia haisemi kwamba Bwana atatubariki!!hapana,  biblia inasema Bwana ameshatubariki kwa  baraka zote katika ulimwengu wa roho.Tunatakiwa kuzibeba baraka zetu kutoka kwenye ulimwengu waroho na kuzilieta kwenye ulimwengu wa mwili.

Waefeso 1:18
"Macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wake katika watakatifu jinsi ulivyo ;kwa kadiri ya utendaji wa nguvu za uweza wake.

JINSI YA KUVILETA VITU KATIKA ULIMWENGU WA MWILI.
MAOMBI:


Katika swala la kutawala siyo kitu kirahisi kama unavyofikilia.
Ni lazima ujitoe hasa kwa kudhamilia kabisa kufanya maombi.Kumbuka ukiomba maombi kama haya ina maana umeanzisha vita na shetani. Sasa usipozivaa silaha sawa sawa unaweza ukashindwa.
Lakini vita vyetu ni vya kiroho wala siyo kimwili.

WAEFESO 6:10-12
10 Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake.
 11 Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.
 12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
We fikiria unapigana na kitu ambacho hukioni.
Efeso 6 Inasema vita vyetu si katika damu na nyama bali katika ulimwengu wa roho. Kwa hiyo lazima kupigana hasa katika maombi ili uweze kutawala ulimwengu wa roho. Maombi haya lazima yawe ya kina yaani muda mrefu hasa majira ya usiku kuanzia saa sita usiku hadi saa tisa. Ukifanya hivi kwa mfululizo hakika utaona mambo umeyatawala.

Kumbuka maombi yako lazima yaambatane na vitu vifuatavyo:-

UTAKATIFU
ISAYA 59:1~2
1 Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia;
 2 lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.

 

IMANI
YAKOBO 1:5~6
 5 Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.
 6 Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku.

 

MATHAYO 17:20
 20 Yesu akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu.
 

BIDII
YAKOBO 5:17
17 Eliya alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi, akaomba kwa bidii mvua isinyeshe, na mvua haikunyesha juu ya nchi muda wa miaka mitatu na miezi sita

NENO LA MUNGU
YOHANA 15:7
7 Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa. 
Unatakiwa kufahamu kuwa katika ulimwengu wa roho umepewa kumiliki vyote,tumepewa kumiliki vyote katika ulimwengu wa roho,tunatakiwa kutumia mamlaka tuliyonayo kuhakikisha tunamiliki kwasababu  tushaandikiwa kushinda katika ulimwengu wa roho.

LUKA 10:19
"Tazama nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge na nguvu zote za yule adui wala hakuna kitu kinahoweza kuwadhuru"

Ushindi wetu uko katika ulimwengu wa roho na tunatakiwa tusababishe uje mwilini.unatakiwa kupambana katika maombi na kuhakikisha vile ulivyonavyo rohoni vinatokea katika ulimwengu wa roho,Yesu alishalipia kila kitu tunachokihitaji.

2WAKORINTHO 8:9.
9 Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.
 
Unapogundua vitu vyako viko katika ulimwengu wa roho ni jukumu letu kuvidai mpaka vitokee mwilini,

2Wakorintho 4:3-4-
Ambao ndani yao Mungu wa dunia hii amepofusha fikra zao wasioamini isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.
Silaha kubwa ya shetani kwa mkristo ni kwa kumzuia asione anachotakiwa kuona anavyostahili kupokea.Shetani anao uwezo wa kupofusha fikra na mawazo na kukufanya usiyaone yale Mungu aliyokusudia kwako.

WARUMI 12:1-2
“Bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema ya kumpendeza na ukamilifu.
Unapookoka unatakiwa kubadilisha namna ya kuwaza,na namna moja ya kuwaza ni kwamba hatushindwi hata siku moja,na baada ya kugeuza namna ya kuwaza ndio utayajua mapenzi ya Mungu yaliyo mema katika maisha yako.Ukigeuzwa upya nia yako ndio utaanza kujua kumbe ni mapenzi ya Mungu wewe usiwe mgonjwa,ni mapenzi ya Mungu ufanikiwe.
By Faraja Euphrase





15 comments:

Anonymous said...

Nimebarikiwa Sana na masomo haya ubarikiwe sana mtumishi Kwa neno hili

Anonymous said...

Nilipata shida Sana kutambua au kufaham maana ya ulimwengu wa roho, hatimaye nimepata kujua.

Anonymous said...

Barikiwa Sana mtu wa baba

Anonymous said...

Ubarikiwe Sana, umeeleza Kwa ufupi na umeeleweka Sana

Anonymous said...

Ubarikiwe 🙌🙌

Anonymous said...

Asante mtumishi nimekuelewa Kwa ukubwa sana

Anonymous said...

Ubarikiwe

Anonymous said...

Amina, Barikiwa sana iwe kwetu kama Neno linenavyo

Anonymous said...

Hakika umefanyika daraja

Anonymous said...

Amina sana mtumishi

SALVATION HOUR said...

Ubarikiwe sana Mtumishi

Anonymous said...

Amina asante kwa ufafanuzi mzuri wa ulimwengu wa roho

Anonymous said...

Abarikiwe nimejifunza kitu

Anonymous said...

Mbarikiwa ongezeka sana

Anonymous said...

🔥

 

Top

Back To Top
 
Blogger Templates