Karibu mwana wa MUNGU tujifunze. Leo tunaangalia somo linasema KUUTAWALA KWANZA ULIMWENGU WA ROHO.
Nini maana ya ulimwengu wa roho?
Ulimwengu wa roho ni ulimwengu usioonekana kwa macho ya damu
na nyama. Ulimwengu wa roho ni ulimwengu halisi kama ilivyo hii dunia. Mapepo,
majini yanaishi katika huo ulimwengu ndiyo maana huwa hatuyaoni. Wachawi na
waganga hufanikisha mambo yao kwa namna ya rohoni yaani katika ulimwengu wa
roho.
Mungu huongea na watu wanaoona,ndiyo sababu Mungu kwenye
biblia alikua anakawaida ya kuwauliza watu unaona nini. Kutawala kunaanzia
kwenye ulimwenguu wa roho na kushindwa pia kunaanzia katika ulimwengu
roho. Hapa namaanisha kila kitu huanzia katika ulimwengu wa roho kabla
hakijadhihirika katika ulimwengu wa damu na nyama.
Waebrania 11:3
"Kwa Imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno
la Mungu hata vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri"
Kila vinavyoonekana vimetokana na vile
visivyoonekana,mafanikio ya mwilini yanatokana na mafanikio yaliyoanzia kwenye
ulimwengu usioonekana yaani ulimwengu wa roho.Ndiyo sababu vile visivyooonekana
ni vya kudumu milele na vinavyoonekana ni vya muda tu.
2 Wakorintho 4:16-18 “…tusiviangalie vinavyoonekana,bali
visivyoonekana.kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu,bali visivyoonekana ni
vya milele"
Tuangalia sasa katika Uumbaji wa Mungu, Je? Adamu alianzia
wapi?
Mwanzo 1 : 26 - Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano
wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na
wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
Mwanzo 1 : 27 - Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano
wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.
Mwanzo 2 : 7 - Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya
ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.
Tumeona mara ya kwanza MUNGU aliwaumba me na ke. (Mwanzo
1:26~27). Alafu katika andiko la pili ndipo tunaona sasa MUNGU anamfanya mtu
kwa mavumbi (udongo). Hapa sasa ndipo tunaona mtu anakuwa katika mwili. (MWANZO
2:7).
Kumbuka uyo mtu MUNGU alimuita Adamu.
MWA 1:27, tumeona MUNGU aliumba me na ke. Je? Adamu alikuwa
na jinsia gani?
Kwa maadiko yale mawili, inadhihirisha kuwa kuwa Adam wakati
amekuwa katika mwili alikuwa na jinsia mbili
Namaanisha hivi ke ilikuwa ndani ya me lakini katika
ulimwengu wa roho
Ndiyo maana sasa baadae tunaona baada ya MUNGU kuona Adam
hana msaidizi alitwaa ubavu mmoja kwa Adamu akamfanya mwanamke, ambaye ni Hawa.
Hadi hapo sasa tumeona hata mwanadamu alianzia katika
ulimwengu usioonekana.
Kwa kifupi naweza kusema kuwa, mwanadamu halisi ni roho
(maana ndiyo iliyoanza kuumbwa MWA 1:27). Huu mwili ulionao umeibeba tu ile
roho.
Angalia andiko hili.
Na kila roho
isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu. Na hii ndiyo roho ya mpinga Kristo ambayo
mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani.
1YOH 4:3
Point yangu ipo hapo kwenye "kila roho isiyomkiri YESU
haitokani na MUNGU".
Ndiyo maana nasema mwanadamu halisi ni yule wa ndani
asiyeonekana, maana mtu anaweza kwa nje akakwambia nampenda YESU, lakini kumbe
rohoni mwake hana YESU.
Kwa hiyo kama mwanadamu ni roho, na kila kitu kinaanzia
rohoni, basi hata baraka zako zinaanzia rohoni, mafanikio yako yananzia rohoni,
uzima wako pia ni katika roho nk.
Kama ndivo ilivyo, ni lazima tuhakikishe tunautawala
ulimwengu wa roho.```
Waefeso 1 : 3 - Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo,
aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake
Kristo;
3 Yohana 1:2
Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na
kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo.
Ukiviangalia vile visivyoonekana tunapata ufumbuzi wa milele
na tunapoviangalia vile vinavyoonekana tunapata ufumbuzi wa muda tu.Vitu
vinavyoonekana vinakua na ufumbuzi wa muda tu lakini vitu vile visivyoonekana
vinakawaida ya kutokua na mipaka.
1Wakorintho 2:9
"lakini kama ilivyoandikwa,mambo ambayo jicho
halikuyaona wala sikio halikuyasikia (wala hayakuingia katika moyo wa
mwanadamu). Mambo hayo Mungu aliwaandalia wampendao."
Mambo ambayo hata hujawahi kuyawaza wala jicho halijawahi
kuyaona, mambo hayo Bwana amewaandalia wampendao, Kama vitu vinaanzia kwenye
kutokuonekana tunatakiwa kung’ang’ania kwenye vile visivyoonekana ili kupokea
majibu yetu yenye kuonekana.
Yeremia 1:11
Tena neno la Bwana likanijia kusema, Yeremia, waona nini?.
Nikasema ninaona ufito wa mlozi, ndipo Bwana akaniambia umeona vema, kwa maana
ninaliangalia neno langu ili nilitimize.
Bwana anaongea na wale wanaoona vitu,ukiona ushindi,ushindi unatokea kwako,ukiona ufumbuzi ufumbuzi unatokea kwako,ukiona taabu, taabu inatokea kwako.
Bwana anaongea na wale wanaoona vitu,ukiona ushindi,ushindi unatokea kwako,ukiona ufumbuzi ufumbuzi unatokea kwako,ukiona taabu, taabu inatokea kwako.
Hata vita tunayopigana ni katika ulimwengu usioonekana,
mambo yasiyoonekana yanasababisha mambo yanayoonekana.
Waefeso 6:12
“kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na
nyama….katika ulimwengu waroho”
Unaposhinda rohoni ushindi unaonekana mwilini na unapopigwa
rohoni na mwilini unashindwa, kwa sababu majeshi tunayopambana nayo yako katika
ulimwengu wa roho.
NAFASI YAKO ROHONI.
Kila mtu aliyeokoka anayo nafasi yake katika ulimwengu wa
roho,
Waefeso 1:3
“…aliyetubariki kwa Baraka zote za rohoni katika ulimwengu waroho katika Kristo Yesu.
“…aliyetubariki kwa Baraka zote za rohoni katika ulimwengu waroho katika Kristo Yesu.
Hatuhitaji kumwambia Mungu atubariki kwasababu Mungu
ameshatubariki kwa baraka zote katika ulimwengu wa roho, biblia haisemi kwamba
Bwana atatubariki!!hapana, biblia inasema Bwana ameshatubariki kwa
baraka zote katika ulimwengu wa roho.Tunatakiwa kuzibeba baraka zetu
kutoka kwenye ulimwengu waroho na kuzilieta kwenye ulimwengu wa mwili.
Waefeso 1:18
"Macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito
wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wake katika watakatifu jinsi ulivyo
;kwa kadiri ya utendaji wa nguvu za uweza wake.
JINSI YA KUVILETA VITU KATIKA ULIMWENGU WA MWILI.
MAOMBI:
Katika swala la kutawala siyo kitu kirahisi kama
unavyofikilia.
Ni lazima ujitoe hasa kwa kudhamilia kabisa kufanya
maombi.Kumbuka ukiomba maombi kama haya ina maana umeanzisha vita na shetani.
Sasa usipozivaa silaha sawa sawa unaweza ukashindwa.
Lakini vita vyetu ni vya kiroho wala siyo kimwili.
WAEFESO 6:10-12
10 Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake.
11 Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.
12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
11 Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.
12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
We fikiria unapigana na kitu ambacho hukioni.
Efeso 6 Inasema vita vyetu si katika damu na nyama bali
katika ulimwengu wa roho. Kwa hiyo lazima kupigana hasa katika maombi ili uweze kutawala ulimwengu wa roho. Maombi haya lazima yawe ya kina yaani muda mrefu hasa majira ya usiku kuanzia saa sita usiku hadi saa tisa. Ukifanya hivi kwa mfululizo hakika utaona mambo umeyatawala.
Kumbuka maombi yako lazima yaambatane na vitu vifuatavyo:-
✍ UTAKATIFU
ISAYA 59:1~2
1 Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia;
2 lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.
2 lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.
✍IMANI
YAKOBO 1:5~6
5 Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.
6 Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku.
6 Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku.
MATHAYO 17:20
20 Yesu akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu.
✍ BIDII
YAKOBO 5:17
17 Eliya alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi, akaomba kwa bidii mvua isinyeshe, na mvua haikunyesha juu ya nchi muda wa miaka mitatu na miezi sita
✍ NENO LA MUNGU
YOHANA 15:7
7 Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.
Unatakiwa kufahamu kuwa katika ulimwengu wa roho umepewa
kumiliki vyote,tumepewa kumiliki vyote katika ulimwengu wa roho,tunatakiwa
kutumia mamlaka tuliyonayo kuhakikisha tunamiliki kwasababu tushaandikiwa
kushinda katika ulimwengu wa roho.
LUKA 10:19
"Tazama nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge na
nguvu zote za yule adui wala hakuna kitu kinahoweza kuwadhuru"
Ushindi wetu uko katika ulimwengu wa roho na tunatakiwa
tusababishe uje mwilini.unatakiwa kupambana katika maombi na kuhakikisha vile
ulivyonavyo rohoni vinatokea katika ulimwengu wa roho,Yesu alishalipia kila
kitu tunachokihitaji.
2WAKORINTHO 8:9.
9 Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.
9 Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.
Unapogundua vitu vyako viko katika ulimwengu wa roho ni
jukumu letu kuvidai mpaka vitokee mwilini,
2Wakorintho 4:3-4-
Ambao ndani yao Mungu wa dunia hii amepofusha fikra zao wasioamini isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.
Ambao ndani yao Mungu wa dunia hii amepofusha fikra zao wasioamini isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.
Silaha kubwa ya shetani kwa mkristo ni kwa kumzuia asione
anachotakiwa kuona anavyostahili kupokea.Shetani anao uwezo wa kupofusha fikra
na mawazo na kukufanya usiyaone yale Mungu aliyokusudia kwako.
WARUMI 12:1-2
“Bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua kujua
hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema ya kumpendeza na ukamilifu.
Unapookoka unatakiwa kubadilisha namna ya kuwaza,na namna
moja ya kuwaza ni kwamba hatushindwi hata siku moja,na baada ya kugeuza namna
ya kuwaza ndio utayajua mapenzi ya Mungu yaliyo mema katika maisha
yako.Ukigeuzwa upya nia yako ndio utaanza kujua kumbe ni mapenzi ya Mungu wewe
usiwe mgonjwa,ni mapenzi ya Mungu ufanikiwe.
By Faraja Euphrase
15 comments:
Nimebarikiwa Sana na masomo haya ubarikiwe sana mtumishi Kwa neno hili
Nilipata shida Sana kutambua au kufaham maana ya ulimwengu wa roho, hatimaye nimepata kujua.
Barikiwa Sana mtu wa baba
Ubarikiwe Sana, umeeleza Kwa ufupi na umeeleweka Sana
Ubarikiwe 🙌🙌
Asante mtumishi nimekuelewa Kwa ukubwa sana
Ubarikiwe
Amina, Barikiwa sana iwe kwetu kama Neno linenavyo
Hakika umefanyika daraja
Amina sana mtumishi
Ubarikiwe sana Mtumishi
Amina asante kwa ufafanuzi mzuri wa ulimwengu wa roho
Abarikiwe nimejifunza kitu
Mbarikiwa ongezeka sana
🔥
Post a Comment